NYOTA MWINGINE YANGA SC KUSEPA

BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Aziz Ki taarifa kueleza kuwa anaondoka ndani ya kikosi hicho kuelekea Wydad inaelezwa kuwa kuna nyota mwingine tena anaondoka katika kikosi hicho.

Aziz Ki amekuwa kwenye mwendo mzuri ndani ya Yanga SC akiwa kacheza jumla ya mechi 114 na kutoa pasi 57 za mabao huku akifunga jumla ya mabao 32.

Ni Clement Mzize chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Zamalek ambao wanahitaji kupata huduma yake.

Mshambuliaji huyo kafunga jumla ya mabao 13 kwa msimu wa 2024 kwenye ligi akiwa ni mzawa namba moja mwenye mabao mengi.

Mbali na Zamalek inaelezwa kuwa mabosi wa Kaizer Chiefs wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo ambaye mguu wakwe wenye nguvu ni ule wa kulia na bao lake la kwanza msimu wa 2024/25 alifunga mbele ya Kagera Sugar, Uwanja Kaitaba ambapo alianzie benchi kwenye mchezo huo.

Alipachika bao la pili akitumia pasi ya kiungo mshambuliaji Aziz Ki baada ya dakika 90 ubao ukasoma Kagera Sugar 0-2 Yanga SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.