SINGIDA BLACK STARS HESABU ZAKE KWA SIMBA SC

UONGOZI wa Singida Black Stars umeweka wazi kuwa kwa sasa hesabu zao zote ni kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba SC ambao ni mzunguko wa pili.

Singida Black Stars kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya nne ikiwa imekusanya jumla ya pointi 53 inatarajiwa kumenyana na Simba SC iliyo nafasi ya pili Mei 28 ikiwa ni mchezo wa ligi.

Kete nyingine kwa Singida Black Stars itakuwa dhidi ya Simba SC ambapo mchezo huu utakuwa wa CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali unatarajiwa kuchezwa Mei 31, Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa.

Mshindi wa mchezo huu atakutana na Yanga SC ambaye ni bingwa mtetezi alipata ushindi kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania kwa ushindi wa mabao 2-0.

Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars ameweka wazi kuwa mabadiliko ya mechi hizo awali yamewapa muda wa kufanya maandalizi hivyo wanaamini benchi la ufundi litawapa mbinu wachezaji.

“Kwa mechi zetu za Mei dhidi ya Simba SC mchezo wa ligi ikiwa ni ile Mei 28 na Mei 31 dhidi ya Simba SC mchezo wa CRDB Federation Cup tupo tayari na benchi la ufundi litakuwa na muda wa kufanya maandalizi mazuri.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.