Masau Bwire abainisha wazi kuwa wapo tayari kwa mapambano ndani ya uwanja
Mkwakwani, Tanga dakika 90 za jasho kwa wababe wawili
MASAU Bwire, Ofisa Habari wa JKT Tanzania amesema kuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup dhidi ya Yanga SC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 18 2025, saa 10:00 jioni.
Ni Yanga SC itakuwa dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani Tanga na mshindi wa mchezo atakutana na Simba SC ama Singida Black Stars ambao mchezo wao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.
Masau Bwire amesema kuwa nguvu hawana mashaka na mechi zote ambazo zipo mbele yao ikiwa ni nusu fainali ya CRDB Federation Cup kwa kuwa wapo imara na maandalizi yapo vizuri.
“Sisi tupo imara na nguvu kubwa ni kuona kwamba tunashiriki mashindano ya kimataifa, wapinzani wetu niseme kwamba watatupisha, hao hao ambao tutakutana nao hakika safari hii watatupisha tunahitaji kushiriki mashindano ya kimataifa.
“Wachezaji na benchi la ufundi wote wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri hivyo mashabiki wawe pamoja nasi tunataka kwenda kucheza mashindano ya kimataifa.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.