SIMBA SC KUCHEZA FAINALI KESHO KMC COMPLEX

BENCHI la ufundi la Simba SC limebainisha kuwa litacheza mchezo wao dhidi ya Pamba Jiji Uwanja wa KMC Complex kama fainali ili kuvuna pointi tatu.

Kwenye msimamo ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 63 baada ya mechi 24 inatarajiwa kuwakaribisha Pamba Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu, Fred Felix Mei 8 2025 kwenye msako wa pointi tatu.

Pamba Jiji wamebainisha kuwa hawajasahu mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza kwa ubao kusoma Pamba Jiji 0-1 Simba SC hivyo wapo tayari kusaka ushindi.

Nafasi ya Pamba Jiji kwenye msimamo ni namba 13 baada ya mechi 26 ikiwa imekusanya pointi 27 ipo kwenye mstari wa kucheza play off ikiwa itamaliza msimamo ikiwa hapo msimu wa 2024/25.

Seleman Matola kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Pamba Jiji wanatambua ugumu wake na wataingia kucheza kama fainali kupata matokeo mazuri.

“Tunatambua ugumu kwenye mchezo wetu dhidi ya Pamba Jiji, tutaingia uwanjani kucheza mchezo wetu kama fainali ili kupata pointi tatu kikubwa ni kuendelea pale ambapo tuliishia kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania.”

Kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania kiungo Joshua Mutale alianza kikosi cha kwanza na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofanya majaribio zaidi ya mawili ndani ya 18 huku kipa wa JKT Tanzania Suleiman akioka hatari zaidi ya tatu zilizotoka kwa wachezaji wa Simba SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.