MOHAMED Hussen Zimbwe Jr nahodha wa Simba amewaomba Watanzania waendelee kuwaombe kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Ni Mei 17 2025 wanatarajiwa kuwa ugenini nchini Morocco kumenyana na RS Berkane na Mei 25 2025 watakuwa Dar kwenye fainali ya pili itakayoamua mshindi wa jumla atakayetwaa taji hilo.
Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Aprili 28 ilirejea Dar ikitokea Afrika Kusini ambapo ilikuwa na mchezo wa mkodo wa pili nusu fainali imetinga fainali kwa ushindi wa bao 1-0 Stellenbosch FC.
Mashabiki wengi walijitokeza kuanzia saa 12 jioni na waliongozana na msafara wa Simba SC barabarani kuanzia saa 9 licha ya mvua kunyesha bado walikuwa na shangwe kutokana na hatua ambayo timu yao imefikia.
Zimbwe amesema: “Tumerejea salama tunamshukuru Mungu hii ni fainali ya Watanzania hivyo tunaomba waendelee kutuombea kwenye mechi zetu mbili ugenini na nyumbani hatua ya fainali. Bado kazi inaendelea kwa kuwa hatua hii muda mrefu hatujafika na sasa malengo yetu nikuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.