HIZI HAPA REKODI ZA STELLENBOSCH 0-0 SIMBA SC

NUSU fainali ya pili ya maamuzi Kombe la Shirikisho Afrika iligota mwisho Aprili 27 2025 ilipokuwa Stellenbosch FC 0-0 Simba SC, Simba SC imetinga hatua ya fainali kwa jumla ya bao 1-0 ambalo walipata kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza Uwanja wa Amaan likifungwa na Jean Ahoua dakika ya 44.

Hizi hapa dakika 90 za baadhi ya wachezaji wa timu zote mbili walichofanya uwanjani kwenye msako wa ushindi anga la kimataifa:-

OSCAR

Kipa wa Stellenbosch FC, Oscar Masuluke alikomba dakika 90 mazima na aliokoa hatari dakika ya 73 iliyopigwa na Mpanzu.

NDULI

Nyota Nduli wa Stellenbosch FC alipiga shuti ambalo lilikwenda nje ya lango dakika ya 38. Nyota huyu hakukomba dakika 90 aligotea dakika ya 82 nafasi yake ikichukuliwa na Philander.

PALACE

Palace ambaye aliingia kipindi cha pili dakika ya 63 akichukua nafasi ya Busaka alipiga shuti ambalo lilikwenda kwenye nyavu za Simba ilikuwa dakika ya 77 baada ya wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha Mohamed Hussen kuomba mwambuzi aangali VAR bao hilo lilifungwa kwa kuwa kuna mchezaji alikuwa ameotea.

TOURE

Toure wa Stellenbosch FC alipiga mashuti mawili ambayo yalikwenda nje ya lango ilikuwa dakika ya 39 kwa pigo la kichwa na alipiga shuti ambalo lililenga lago dakika ya 45.

BASADIEN

Basadien wa Stellenbosch FC alipewa majukumu ya  kurusha dakika ya 44, 45. Khiba naye alirusha dakika ya 72.

HAWA HAPA SIMBA SC

Kipa wa Simba Moussa Camara aliokoa hatari dakika ya 36, 45, 45 na kukamilisha dakika za mwanzo lango likiwa salama. Kipindi cha pili Camara aliokoa hatari dakika ya 47, 69,70, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 86 kwa kosa ambalo mwamuzi alitafsiri kuwa alikuwa anapoteza muda.

MUKWALA

Mshambuliaji Steven Mukwala alianza kikosi cha kwanza na alicheza faulo dakika ya 53 aligotea dakika ya 53 nafasi yake ilichukuliwa na Leonel Ateba.

YUSUPH KAGOMA

Kwa kiungo mkabaji Yusuph Kagoma kwenye harikari za kuokoa alicheza faulo dakika ya 36. Kagoma kipindi cha pili alicheza faulo dakika ya 51 alimchezea Titus.

SHOMARI KAPOMBE

Shomari Kapombe alipewa majukumu ya kurusha ilikuwa dakika ya 41, 43. Kapombe aliokoa hatari dakika ya 86. Kapombe kipindi cha pili alirusha dk 48 cheza faulo dk 59, alipiga kona dk 73.

KIBU D

Kibu Dennis alichezewa faulo dakika ya 14 iliamuliwa penati na mwamuzi ikafutwa baada ya kutazama VAR. Kibu alicheza faulo dakika ya 81 na aliokoa hatari dakika ya 88.

MPANZU

Ellie Mpanzu alichezewa faulo dakika ya 45 na Traore. Mpanzu kipindi cha pili alichezewa faulo dakika ya 67, 80. Che Malone aliingia dakika ya 86 kuchukua nafasi ya Mpanzu.

JEAN AHOUA

Jean Ahoua alipewa jukumu la  kupiga faulo dakika ya 45 alipiga kona dakika ya 45. Alichezewa faulo nyingine dakika  45 na Kezy. Kipindi cha pili alichezewa faulo dakika ya 48, 55 na Moloisane. Hakukomba dakika 90 aligotea dakika ya 64 ni Mavambo ambaye mpira wake wa kwanza kupiga ilikuwa dakika ya 65 ulikwenda nje.

HAMZA JR

Hamza Jr aliokoa hatari dakika ya 43, Chamou aliokoa hatari dakika ya 45. Kipindi cha pili Hamza aliokoa hatari dakika ya 67, 68.

ZIMBWE JR

Nahodha Zimbwe Jr alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 49, 62, 64, 69. Beki huyu hakokomba dakika zote 90 aligotea dakika ya 86 Nouma aliingia.

CHAMOU

Nyota wa Simba Chamou alionekana  kucheza faulo dakika ya 54 ambayo iliamuliwa kuwa penati ndani ya 18, VAR ilikataa tukio hilo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.