NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma amebainisha kuwa ana matumaini ya kuona Simba SC inapatata matokeo mazuri kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika unaotarajiwa kuchezwa Afrika Kusini, Aprili 27 2025.
Simba SC inakumbuka kwamba mchezo uliochezwa Tanzania ilipata ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Jean Ahoua inakibarua cha kusaka ushindi wa jumla kwenye dakika 90 za ugenini.
Ipo wazi baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Stellenbosch FC ambao walikuja kwa mbinu yakujilinda zaidi dakika zote 90.
Mshindi kwenye mchezo huo anatarajiwa kucheza fainali na mshindi wa jumla kati ya CS Constatine na RS Berkane ambao nao watashuka uwanjani Aprili 27.
Mwinjuma amesema: “Nimekuja nikiwa na furaha kushuhudia utekelezaji wa mkataba kati ya Simba na Jeyrutty walioingia wiki mbili zilizopita nikiwa mgeni rasmi na nimeshangazwa na jambo hili kutekelezwa kwa haraka kama ilivyoahidiwa. Hongera sana Jeyrutty kwa kuanza mapema utekelezaji.
“Nimekuja kuiwakilisha serikali hapa Afrika Kusini kwa ajili ya kuendelea kuwapa ushirikiano Klabu ya Simba kuhakikisha wanacheza wanafanya vizuri kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili na kwenda fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).
“Niwatakie kila la kheri na ushindi mnono kwenye mechi ya Jumapili ambayo itachezwa kule Durban na katika kipindi cha hivi karibuni hakuna timu inatamani kukutana na Simba na serikali imewapa ushirikiano mkubwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.”