SIMBA KAMILI KIMATAIFA, TAMBO ZATAWALA

SIMBA SC itakuwa kibaruani kusaka ushindi dhidi ya Stellenbosch FC ni mchezo wa nusu fainali ya wababe wawili 2024/25 kimataifa wakiwa na rekodi yakumfungashia virago bingwa mtetezi kwenye mashindano ya kimataifa kwa nyakati tofauti.

Aprili 20 2025 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa uwanja wa New Amaan Complex huku Simba SC ya Tanzania ikiwa na rekodi yakumfangashia virago Zamalek 2003 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Stellenbosch FC wamemfungashia virago Zamalek kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

NENO LA SEMAJI AHMED ALLY

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo na wasiwe na presha kwa timu hiyo kutoka Dar na kwenda visiwani.

“Niwaombe watu wa Zanzibar na hasa mashabiki wa Simba SC wafanye kila kinachowezekana kuipeleka Simba fainali. Nilisema kila kizazi na historia yake, hii imekuja wakati muafaka na sisi kuandika historia ya kuipeleka Simba SC  fainali. Tufanye kila kinachowezekana Mnyama kwenda fainali.

“Mpinzani wetu Stellenbosch FC sio timu dhaifu, hadi inafika hatua hii inaonyesha ni timu ambayo imejiandaa. Wanasimba wote tulijiandaa kucheza na Zamalek lakini Stellenbosch FC akammaliza pale pale nyumbani kwake. Hajamtoa Zamalek kwa bahati mbaya.

“Ni kweli ni timu ngeni lakini ina wachezaji wenye ubora mkubwa na wana kocha mkubwa. Tuna kazi kubwa kwelikweli kuhakikisha tunamthibiti, tunamfunga ili tukienda kwenye mechi ya ugenini ni iyenaiyena hadi fainali.

WALIFIKAJE HAPO

Simba SC ilipita hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya penati 4-1 dhidi ya Al Masry baada ya mchezo wa kwanza ugenini ubao kusoma Al Masry 2-0 Simba, robo fainali ya pili ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 Al Masry hivyo mshindi alipatikana kwa penati.

Stellenbosch FC wao walipata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Zamalek ambao walikuwa ni mabingwa watetezi walitolewa kwa kufungwa bao 1-0 wakiwa nyumbani Aprili 9 2025 baada ya ile robo fainali ya kwanza ubao kusoma 0-0 kwa timu zote mbili Aprili 2.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.