SIMBA YATINGA NUSU FAINALI, YANGA KAZINI

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Fadlu Davids kimetinga hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup kwa ushindi dhidi ya Mbeya City.

Kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Simba ilipata mabao kupitia kwa Fabrince Ngoma dakika ya 24 akiweka usawa bao la Mudathir Said wa Mbeya City aliyepachika bao dakika ya 22.

Bao la pili kwa Simba lilipachikwa na Leonel Ateba dakika ya 38 na kamba ya tatu ilifungwa na Joshua Mutale ambaye alikuwa kwenye kiwango chake katika mchezo huo.

Simba inawafungashia virango Mbeya City ambayo iliwafungashia virago Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Simba Aprili 13 2025 kipindi cha pili ilitengeneza nafasi zaidi ya tatu kupitia kwa Awesu Awesu, Ateba, Edwin Balua  walikwama kuzitumia kwenye mchezo huo.

Mabingwa watetezi Yanga Aprili 15 watakuwa kazini kusaka tiketi yakutinga nusu fainali watamenyana na Stand United.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.