SIMBA imeandika rekodi yake nyingine kwa kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa penati 4-1, baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa, Aprili 9 2025 kusoma Simba 2-0 Al Masry kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza ilikuwa Al Masry 2-0 Simba.
Dalali Mwanamke ametoa zawadi kwa mchezaji bora wa mchezo ambaye ni Moussa Camara aliyeokoa penati mbili na penati ya mwisho ilipigwa na beki Shomari Kapombe.