MKANDAJI KIBU D APATA KITETE ISHU YA KARIAKOO DABI

KIBU Dennis kiungo wa Simba maarufu kwa jina la Kibu Mkandaji amepata kigugumizi kuhusu mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 8 2025.

Mkandaji lilipata umaarufu baada ya kufunga kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa alipomtungua Djigui Diarra kwa shuti kali akiwa nje ya 18 .

Ni Aprili 16 2023 katika Kariakoo Dabi, Kibu alifunga bao moja wakati ubao uliposoma Yanga 0-2 Simba bao lingine lilifungwa na beki Henock Inonga. Katika mchezo huo Kibu alikuwa ni nyota wa mchezo wakati Simba walipokomba pointi tatu mbele ya watani zao wa jadi.

Kete ya kwanza msimu wa 2024/25 iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, ilikuwa Simba 0-1 Yanga, pointi tatu walipoteza Simba ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa wababe hao kupoteza ndani ya ligi.

Kibu ameweka wazi kuwa yeye anapenda kucheza mechi kubwa ambazo zinamfanya atumie nguvu nyingi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wengine jambo linalomfanya awe katika ubora lakini kuelekea mchezo dhidi ya Yanga hakutaka kuzungumza mengi.

“Ni kweli huwa ninapenda mechi ngumu ambazo zinakuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa sina hofu nina tambua kwamba mazoezi ambayo tunayafanya yanatujenga lakini kuelekea mchezo wetu ujao sitasema chochote kwa kuwa tupo kwenye maandalizi na ninaamini mchezo utakuwa mgumu.”

Ndani ya ligi msimu wa 2024/25 Kibu Dennis ni mechi 15 kacheza akikomba dakika 1,020 ni pasi moja ya bao ametoa kwenye mechi za ligi ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.