JOTO la Kariakoo Dabi linazidi kupasua anga ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 mchezao wa mzunguko wa pili.
Ni mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wababe hawa wawili ambapo kila timu imetoka kupata ushindi kwenye mchezo wake uliopita.
Yanga ambao watakuwa nyumbani walishuhudia ubao ukisoma Pamba Jiji 0-3 Yanga wakasepa na pointi tatu mazima huku Aziz Ki akitupia mabao mawili na Boka akitupia bao moja kwa upande wa Simba walishuhudia ubao ukisoma Coastal Union 0-3 Simba na mabao yakifungwa na Steven Mukwala.
Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kuelekea kwenye mchezo huo ambapo mzunguko ni 5,000, machungwa 10,000, VIP C 20,000, VIP B 30,000 ile ya VIP A tayari mzigo umekata mapema.
Mwamuzi wa kati ni Ahmed Arajiga ambaye ametangazwa rasmi Machi 5 2025 kuwa atakuwa pilato kwenye mchezo huo ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.