NYOTA watatu wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids watakosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Machi Mosi 2025 ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Kwenye msimamo Simba ni namba mbili baada ya mechi 20 imekusanya pointi 51 itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union ambayo ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 21.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao ulichezwa Uwanja wa KMC, Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Coastal Union wababe hao waligawana pointi mojamoja na kila timu ikpaoteza pointi mbili.
Ni Mousa Camara ambaye ni mlinda mlango namba moja wa Simba akiwa amecheza mechi 21 akifungwa mabao 8 na amekusanya hati safi 15 akiwa ni kipa namba moja kwenye eneo hilo licha ya makosa ambayo amekuwa akifanya kwenye mechi.
Che Malone ambaye ni beki kiongozi wa kati naye huenda atakosekana kwenye mchezo huo yeye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ilikuwa dakika ya 17 kwenye harakati za kutimiza majukumu yake.
Mzamiru Yassin naye hakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Azam FC lakini hayupo fiti hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Coastal Union ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wapo wachezaji ambao watakosekana lakini bado wapo wachezaji wengine ambao watacheza kutimiza majukumu yao.
“Kuna wachezaji watakosekana kwenye mchezo wetu ikiwa ni Mousa Camara kuna mtikisiko kidogo kwa sababu hajawahi kukosa mchezo hata mmoja kwa hiyo kukosekana kwake kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union kutayumbisha mambo kidogo.
“Kwa upande wa Che Malone watu wengi wapo kwa ajili ya kutimiza majukumu yake tunakumbuka mchezo uliopita aliumia mapema nae neo la walinda milango pia makipa waliopo ikiwa ni Ally Salim na Hussen Abel wote wana uwezo mkubwa.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.