BALAA LA FEI NI ZITO KINOMANOMA

BALAA la kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ndani ya ligi namba nne kwa ubora ni nzito kinomanoma kutokana na mwendelezo wake kuwa imara katika upande wa pasi za mwisho msimu wa 2024/25.

Timu hiyo kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 22 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 45 na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 32 ikiwa ndani ya timu tatu zenye mabao mengi ndani ya ligi.

Fei kahusika katika mabao 16 kati ya 32, akitupia jumla ya mabao manne na yote mguu wake wenye nguvu zaidi ni ule wa kulia kwa kucheka na nyavu na kutoa jumla ya pasi 12 za mabao kwenye ligi.

Pasi yake ya 10 alitoa katika mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dakika ya 65 kwa mguu wake wa kulia alimpa mshikaji wake Gibril Sillah ambaye kwenye mchezo huo uliochezwa Februari 6 2025 aliibuka kuwa mchezaji bora.

Alitoa pasi ya 11 kwa mguu wa kulia akimpa Zidane Sereri kwenye Mzizzima Dabi Februari 24 2025 mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa dakika ya 88 pasi iliyopewa thamani ya dola milioni na Mkuu wa Idara ya Habari Azam FC, Zakaria Thabit.

Pasi yake ya 12 alitoa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo dakika ya 43 akimpa mshikaji wake Sillar walipotoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo, Uwanja wa Azam Complex.

Fei amekuwa na zali dhidi ya KMC kwa kuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa KMC Complex Septemba 19 2024 alitoa pasi yake ya kwanza dakika ya 19 alimpa Nado na katika mchezo huu yeye alichaguliwa kuwa mchezaji bora alitoa pasi mbili zilizoleta mabao nyingine alimpa Lusajo dakika ya 54.

Bao lake la kwanza msimu wa 2024/25 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold ilikuwa Oktoba 25 2024 dakika ya 19 Uwanja wa Azam Complex kwa pigo la penalti.

Bao la pili aliwatungua Kagera Sugar dakika ya 55 Azam Complex kwa pigo la penalti, bao la tatu aliwatungua Singida Black Stars dakika ya 37 Azam Complex na bao la nne aliwatungua Dodoma Jiji ilikuwa Desemba Mosi 2024 kwa pigo la penalti.

Mabao matatu kafunga kwa penalti kati ya manne aliyonayo kiungo huyo ambaye ametumia mguu wa kulia kufunga mabao yote hayo ndani ya ligi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.