SIMBA YAWAFUATA COASTAL UNION KAMILI

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kimekwea pipa kuelekea Arusha kwa maandalizi ya mwisho kuikabili Coastal Union wakiwa kamili gado kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ipo wazi kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Coastal wakigawana pointi mojamoja na langoni alikaa Mousa Camara ambaye ni kipa namba moja wa Simba.

Camara hayupo fiti kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union baada ya kupata maumivu mchezo dhidi ya Azam FC ambao waligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2.

Ikumbukwe kwamba mchezo dhidi ya Coastal Union ilikuwa ni sare ya kwanza kwa wababe hao ndani ya ligi namba nne kwa ubora, mchezo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Machi Mosi 2025 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Miongoni mwa wachezaji waliopo katika msafara huo ni Shomari Kapombe, Hamza Jr, Joshua Mutale, Kibu Dennis, Fabrince Ngoma.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.