AZAM FC WABANWA MBAVU AZAM COMPLEX

WAUAJI wa Kusini, Namungo wamesepa na pointi moja Azam Complex ubao uliposoma Azam FC 1-1 Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho katika kuvuja jasho dakika 90.

Bao la mapema kwa Namungo lilifungwa na Hamis Halifa dakika ya 12 akiwa nje ya 18 akitumia pasi kutoka kwe Legend, Jacob Masawa aliyempa kwa mguu wa kulia likawekwa usawa na Gibril Sillar akiwa ndani ya 18 dakika ya 43.

Sillar kwenye mechi mbili mfululizo ametupia alianza kwenye mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo alitupia bao la mapema kabisa dakika ya kwanza katika Mzizima Dabi baada ya kipa Camara kutema mpira alioupiga mara ya kwanza akiwa ndani ya 18.

Ni pasi ya kiungo Feisal Salum alitumia katika mchezo huo ikiwa ni pasi ya 12 kwa kiungo huyo ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Pointi moja inawajengea ngome Azam FC kwenye nafasi ya tatu wakiwa  na pointi zao ni 45 huku Namungo ikiwa nafasi ya 12 pointi 23 zote zimecheza mechi 22.

Shukrani kwa Jonathan Nahimana ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.