YANGA YAMALIZANA NA SINGINDA BLACK STARS

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize amechaguliwa kuwa mchezaji bora katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Ubao umesoma Yanga 2-1 Singida Black Stars kwa mabao ya Mzize dakika ya 14 alifikisha mabao 10 akiwa kinara katika chati ya utupiaji Bongo.

Bao la pili ni mali ya Prince Dube ambaye amepachika bao hilo kwa kichwa akiwa ndani ya 18 akimalizia pigo la kona ya Maxi Nzengeli.

Bao pekee la Singida Black Stars limepachikwa dakika za jioni na Jonathan Sowah ambaye alitumia makosa ya kipa Djigui Diarra kutema mpira ndani ya 18 ikiwa ni krosi iliyopigwa na Edmund John.

Katika mchezo mwingine Fountain Gate imetoshana nguvu na Tabora United kwa ubao kusoma 0-0. Mwamuzi katika mchezo huu alikuwa ni Hance Mabena na ule dhidi ya Yanga Saad Mrope.

Pointi 52 nafasi ya kwanza Yanga baada ya kucheza jumla ya mechi 20 Singida Black Stars wanabaki na pointi 37 baada ya mechi 20.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.