Jonathan Sowah amefunga bao lake la pili la msimu kwenye mechi yake ya pili kwenye Ligi Kuu bara akiiandikia Singida Black Stars bao la ushindi katika Dimba la Meja Jenerali Isamuyo dhidi Maafande wa JKT Tanzania ambao waliikazia Yanga Sc kwenye mchezo uliopita na kuondoka na alama moja kwenye dimba hilo.
Singida Black Stars wanaendelea kusalia nafasi ya nne pointi 37 baada ya mechi 19 huku JKT Tanzania wakisalia nafasi ya 10 pointi 20 baada ya mechi 19.
FT: JKT Tanzania 0-1 Singida Black Stars
⚽ 52’ Sowah