MKUTANO MKUU WA KAWAIDA WA CECAFA KUFANYIKA KESHO JUBA

Mkutano huo utakaohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 utafanyikia katika hoteli ya Imperial Plaza mjini Juba.

Auka John Gecheo, Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA alithibitisha kuwa Rais wa WAFU A, Bajo Lamin Kaba, Rais UNIFAC, Maolas Jean Guy Blaise na makamu wa Rais wa WAFU B Gasua Ibrahim Musa watakuwa miongoni mwa wageni katika mkutano huo.

Mbali na Marais na Makatibu Wakuu wa nchi 12 Wanachama wa CECAFA watakaohudhuria mkutano huo, CAF pia itawakilishwa na mkuu wa vyama vya wanachama, Sarah Mukuna na Genan Muhamed.

Rais wa shirikisho la Soka la Niger, Djibrilla Hima Hamidou, maofisa wawili kutoka FIFA, pia watahudhuria. Rais wa Vilabu Afrika (ACA), Eng. Hersi Said pia atapamba mkutano huo.

Mkutano huo utajadili mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mashindano ya CECAFA kwa 2024 na kalenda ya 2025-2026.

CECAFA chini ya uongozi wa Wallace Karia ina wajumbe 12; Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Eritrea, Somalia, Djibouti, Ethiopia, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan na Zanzibar.