YANGA WAGAWANA POINTI MOJA KIMATAIFA, GUSA ACHIA YAKWAMA

MCHEZO wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya MC Alger umegota mwisho huku mpango kazi wa Gusa achia twende robo fainali kwa Yanga ukikwama kwa wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa katika anga la kimataifa.

Yanga katika mchezo wa leo ilikuwa inahitajika kupata ushindi baada ya dakika 90 ubao Yanga 0-0 MC Alger. Yanga inabaki nafasi ya tatu na pointi 8 huku MC Alger nafasi ya pili na pointi 9 wakitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mchezo wa leo kundi A ni jumla ya mashuti 18 Yanga walipiga kuelekea langoni mwa wapinzani wao MC Alger huku matatu yakilenga lango katika mchezo wa leo ambao wapinzani wao walikuja kwa mpango kazi wa kujilinda zaidi.

MC Alger rekodi zinaonyesha kuwa ni mashuti matatu pekee walipiga kuelekea langoni huku shuti moja pekee likilenga lango kwenye mchezo huo.

Yanga ilipata jumla ya kona 14  kwenye mchezo na MC Alger ni kona moja pekee walipata ikiwa inamaanisha kwamba Yanga walikuwa wakishambulia zaidi kwenye lango la wapinzani katika msako wa ushindi.

Nyota watatu wa MC Alger walionyeshwa kadi za njano huku Yanga wakiwa salama ndani ya dakika 90 na hakuna kadi nyekundu iliyoonyeshwa kwenye mchezo.

AL HILAL WAPOTEZA KIMATAIFA

TP Mazembe 4-0 Al Hilal ambapo mabao ya TP Mazembe yamefungwa na Diof dakika ya 22, Keita dakika ya 29, Vundi dakika 58 na Shaiu dakika ya 89 kwa mkwaju wa penalti.

Al Hilal nafasi ya kwanza na pointi zao ni 10

MC Alger nafasi ya pili pointi 9

Yanga kutoka Tanzania nafasi ya tatu na pointi 8

TP Mazembe nafasi ya nne pointi zao ni 5

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.