Mshambuliaji wa kimataifa wa Congo DR na klabu ya Pyramids FC ya Misri Fiston Mayele, anashuka dimbani leo kusaka tiketi ya kuwania kufuzu hatua ya Robo Fainali akiwa ugenini dhidi ya klabu ya Sagrada Esperanca ya Angola.
Pyramids atatinga rasmi katika robo fainali ya michuano hiyo kama atapata ushindi wowote na kufikisha alama 10 katika kundi D kabla ya mchezo wao wa mwisho ambao watakuwa nyumbani.
Mayele ana uchu mkubwa wa kuiona timu yake ikifuzu kwani nyota huyo amekuwa na wakati mgumu katika michuano ya ligi ya Mabingwa Barani Afrika tangu akiwa na Yanga licha ya kucheza fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Ifahamike kuwa Mayele alishindwa kutoboa hatua ya makundi msimu jana na alitoa ugwadu wake nchini Ivory Coast ambako alicheza nusu fainaili ya michuano ya AFCON akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Congo DR.