MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamegawa dozi ya 4G kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC Bank.
Ni Merry Christmas 2024 ambapo Dodoma Jiji ni mashuti matatu pekee yaliyopigwa na kulenga lango huku Yanga mashuti matano na manne yalijaa nyavuni.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma umesoma Dodoma Jiji 04 Yanga Clement Mzize katupia mawili dakika ya 18 na dakika ya 37 kwenye mchezo huo, moja limefungwa na Aziz Ki kwa mkwaju wa penalti dakika ya 28 likiwa ni bao lake la pili ndani ya ligi na kamba ya nne mali ya Prince Dube dakika ya 62 akifikisha jumla ya mabao matano.
Yanga inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 nafasi ya pili kwenye msimamo na vinara ni Simba wenye pointi 37 baada ya kucheza mechi 14.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.