AHOUA MKALI KWA KUCHEKA NA NYAVU ATOA ZAWADI YA CHRISTMAS

MWAMBA Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba ambaye bado hajawa imara ndani ya uwanja kwenye mechi ngumu amekuwa ni mkali wa kucheka na nyavu msimu wa 2024/25 katika kikosi cha Simba.

Desemba 24 dhidi ya JKT Tanzania iliyokuwa imara kwenye ulinzi alifunga bao moja dakika za jioni akifikisha mabao 7 ndani ya ligi akiwa ni kinara wa utupiaji kwa nyota wa Simba.

Katika mchezo huo kipa Yakoub Suleiman alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo baada ya kuokoa hatari zaidi ya tano katika mchezo huo zilizopigwa na Leonel Ateba, Ellie Mpanzu, Awesu Awesu, Mukwala ngoma ilikuwa nzito kwa Simba na ngome ya JKT Tanzania kuwa salama.

Ikumbukwe kwamba Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba aliweka wazi kwamba Ahoua amekuwa akikuzwa na vyombo vya habari ila bado ni mchezaji anayehitaji muda zaidi kuwa bora.

Bao lake dakika ya 90+3 dhidi ya JKT Tanzania kwa mkwaju wa penalti linamfanya afikishe mabao 7 ndani ya ligi na pasi nne za mabao akiwa ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu ndani ya Simba kinara ni Elvis Rupia kwenye ligi ana mabao 8.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.