SIMBA imeibuka na ushindi wa bao 1-0 JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wq KMC, Complex. Ni zawadi ya Christmas mapema leo Desemba 24 ambapo Wakristo duniani watakuwa kwenye ibada ya Usiku Mtakatifu na Christmas itakuwa Desemba 25, siku ya kufungua zawadi ni Desemba 26.
Bao la ushindi limefungwa na Jean Ahoua kwa pigo la penalti dakika ya 90+3 baada ya mchezaji wa JKT Tanzania kumchezea faulo Shomari Kapombe.
Ni Ahoua alianzia benchi aliingia dakika ya 45 alichukua nafasi ya Awesu Awesu na Ellie Mpanzu alikomba dakika 59 nafasi yake aliingia Joshua Mutale, Mukwala naye aliingia akichukua nafasi ya Ateba.
Kipa wa JKT Tanzania pongezi kwake Yakoub Suleiman alitimiza majukumu yake kwa kuokoa hatari zaidi ya 5 ikiwa ni dakika ya 17, 37, 53, 53, 54 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 70.
Nyota wa JKT Tanzania, Mohamed Bakari alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Mchezo mwingine uliochezwa mapema Desemba 24 ilikuwa Singida Black Stars 2-1 Ken Gold mabao yakifungwa na Arthur Bada dakika ya 46, Elvis Rupia dakika ya 55 na bao la Ken Gold likifungwa na Herbert Lukindo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.