
Aliyekuwa Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba, Dkt. Anorld Kashembe amefariki Dunia leo Desemba 23, 2024 huku klabu hiyo ikielezea kusikitishwa kumpoteza CEO wao huyo wa zamani ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa klabu hiyo.
“Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya msiba uliotokea leo 23.12.2024 wa aliyekuwa Mtendaji wa klabu Dk Anorld Kashembe” imesema taarifa ya leo Desemba 23, 2024 iliyotolewa na klabu hiyo.
Dkt. Kashembe ambaye alikuwa CEO wa Simba kuanzia 2019 hadi 2021 aliiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa yakiwemo kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu na moja la Shirikisho Tanzania huku timu ya wanawake ya Simba ‘Simba Queens’ ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.