SIMBA ni timu ambayo imefunga mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kucheza jumla ya mechi 13 ndani ya NBC Premier League.
Mabao 29 imefunga huku kinara wa utupiaji akiwa nj Jean Ahoua mwenye mabao sita kibindoni kwenye ligi.
Ateba na Mukwala hawa wawili wametupia mabao mannemanne kila mmoja katika mabao hayo 29.
Ikumbukwe kwamba Simba ni timu ya kwanza kufunga mabao mengi katika mzunguko wa kwanza ilikuwa ni Desemba 21, Kagera Sugar 2-5 Simba.
Imefungwa mabao machache uwanjani ambayo ni matano huku Camara akiwa hajafungwa kwenye mechi 10.
Ukiweka kando kuwa timu ambayo imefungwa mabao machache inaogoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2024/25 baada ya mechi 13 ni pointi 34 imekusanya inafuatiwa na Azam FC nafasi ya pili yenye pointi 33 baada ya kucheza mechi 15.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.