MSHAMBULIAJI wa Simba Leonel Ateba ameweka wazi kuwa watapambana kutafuta ushindi kwenye mchezo wa kimataifa unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Desemba 8 2024.
Simba kwa sasa ipo nchini Algeria kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya CS Constantine ambapo ni Aishi Manula aliyekuwa kwenye mpango wa safari alipata changamoto ya kiafya hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi hicho.
Unakuwa ni mchezo wa pili kwa Simba katika hatua ya makundi baada ya ule wa kwanza kupata ushindi dhidi ya Bravos kwa bao 1-0 mtupiaji akiwa ni Jean Ahoua kwa pigo la penalti.
Ateba amesema kuwa sio mchezo mwepesi lakini watapambana kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo amba oni muhimu wao kupata ushindi.
“Mchezo hautakuwa mwepesi tunaamini ushindani ni mkubwa na mpinzani wetu naye anahitaji matokeo hivyo tutaingia uwanjani kwa mbinu za mwalimu na malengo ni kuona tunapata matokeo mazuri.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.