KHALID AUCHO AFANYA MAZOEZI YA KUJIWEKA SAWA DHIDI YA MC ALGER

Kuelekea mchezo wa pili wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya klabu ya Yanga Sc dhidi ya MC Alger ya Algeria, kiungo wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho ameonekana akifanya mazoezi ya kujiweka sawa huku amiwatoa wasiwasi Wananchi kwa kudai yupo ‘fresh’

Kupitia video fupi iliyowekwa kwenye ukurasa wa mitandao ya kijamii wa klabu hiyo, Aucho ambaye amekosekana katika mechi kadhaa kutokana na majeraha amesema “Niko fresh naendelea na mazoezi ”

Baada ya kukosekana kwa majeraha nyota huyo amejumuhishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo katika safari ya kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo huo. Yanga ilipoteza 2-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudani kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.