SIMBA YAANZA KWA USHINDI LIGI KUU BARA

SIMBA imeeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili ambapo Tabora United waliingia uwanjani kwa hesabu za kujilinda zaidi huku wakifaya mashambulizi kwa kushtukiza mbele ya Simba.

Mabao yamefungwa na Che Malone dakika ya 14, Valentino Mashaka dakika ya 67 na msumari wa mwisho kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ukipachikwa kimiani na Awesu Awesu dakika ya 90.

Awesu ambaye ni ingizo jipya ndani ya Simba alikuwa na siku nzuri kazini ndani ya uwanja kutokana na kazi aliyofanya kuituliza timu na kutengeneza nafasi ndani ya uwanja.

Kipa wa Tabora United, Haroun Mandanda alikuwa na kazi uwanjani kuokoa hatari za washambuliaji wa Simba ndani ya dakika 90 uwanjani.