AZAM FC KAMILI KUPEPERUSHA BENDERA KIMATAIFA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Azam FC wamebainisha kwamba wapo tayari kwa mchezo wao kesho hatua ya awali dhidi ya APR.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex ambapo Azam FC itawakaribisha APR kutoka Rwanda kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Bruno Ferry amesema kikubwa ambacho wanahitaji ni kupambana na kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataia kwa kufanya kwa kweli kuonesha walistahili kuwa hapo.

“Tulipambana kweli kuwa hapa na kupata hii nafasi hilo lipo wazi na tumefanikiwa  kupata fursa ya kuliwakilisha taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa tunapaswa kuonesha kwa vitendo ya kwamba kweli tulistahili kuipata hiyo nafasi na kesho tutaanza kulionesha jambo hilo.

Nahodha wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda amebainisha kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo na wana amini watapata matokeo mazuri uwanjani.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani tunaamini tunakwenda kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afika. Kwa upande wa wachezaji tupo vizuri.”

Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi cha Azam FC ni Feisal Salum, Yannick Bangala, Nado.