AZAM FC YATUMA UJUMBE MZITO

UONGOZI wa Azam FC umetuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao kitaifa na kimataifa kwa kubainisha kuwa watawashangaza wengi kwenye mechi za ushindani.

Ikumbukwe kwamba Azam FC imegotea nafasi ya pili kwenye Ngao ya Jamii 2024/25 baada ya kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa kwa kushuhudia ubao ukisoma Yanga 4-1 AzamFC.

Kwenye mchezo huo Azam FC ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wa zamani wa Yanga Feisal Salum mapema dakika ya 13 liliwekwa usawa na mshambuliaji Prince Dube na mwisho wakapoteza taji la Ngao ya Jami.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa wanatambua ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa kwa timu zote licha ya kuwa bora walipoteza lakini wasichukuliwe poa na wapinzani wao.

“Wapinzani wetu wasituchukulie poa wanaoa kwamba tumefungwa mabao manne na Yanga wasiamini kwamba wanaweza kutufunga nao pia mabao hayo kwani yale yalikuwa ni makosa na tumepoteza licha ya kwamba tulikuwa bora.

“Azam FC tuna timu bora na tunakwenda kufanyia kazi makosa ambayo yalipita hivyo wanavyokuja kwetu waje kwa tahadhari wasifikiri kufungwa ubora umeondoka hapana ubora wetu upo palepale.”

Katika ligi msimu wa 2023/24 Azam FC iligotea nafasi ya pili itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.