MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamerejea Dar mapema kabisa wakiwa na kombe walilotwaa Rwanda mbele ya Rayon Sports iliyowaalika ambapo siku hiyo ilikuwa rasmi kwa timu hiyo kufanya utambulisho wa wachezaji kuelekea msimu wa 2024/25.
Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo ilitwaa ubingwa wa Kombe ka Choplife baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Agosti 4 2024.
Ni bao la Lusajo Mwaikenda dakika ya 56 akitumia pasi ya Tiesse Frank katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja.
Agosti 8 2024 Azam FC inayoshiri Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Fainali itakuwa Uwanja wa Mkapa Agosti 11 2024 ikiwa ni mwanzo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2024/25. ambapo mabingwa watetezi ni Yanga walitwaa taji hilo wakiwa na pointi 80 kibindoni.