MUASISI SIMBA DAY AFICHUA SABABU YA WAZO, MO NDANI KWA MKAPA

MUASISI wa Simba Day Hassan Dalaliambaye alikuwa mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo ameweka wazi kuwa wazo lakuanzisha tamasha hilo lilikuja wakati wakiwa hawana hela kwa ajili ya kulipia Uwanja wa Bunju ambao kwa sasa unaitwa Mo Arena.

Dalali amesema kuwa walikuwa hawana hela ya kulipa uwanja jambo ambalo likamfanya afikirie namna ya kupata fedha kukamilisha mpango wa kulipa kwa kuwa ilikuwa ni fedha nyingi.

“Mimi ni muasisi wa Simba Day nakumbuka ilikuwa mwaka 2007  hatukuwa na hela ya kulipa kwa wakati huo ilikuwa inahitajika milioni 107 hivyo nikawaza kwa nini tusiwe na Simba Day?Mashabiki waje waone jezi mpya wawaone wachezaji wao lakini fedha ambazo zitapatikana zianze kupunguza gharama za kiwanja?

“Hapo tukaanza wazo hilo na ninamshukuru Mungu imekuwa vizuri na linaingia kwenye orodha ya maamasha makubwa duniani ukiacha Kombe la Dunia Simba Day linaingia namba nne hivi kutokana na kupokelewa vizuri.’ amesema.

Leo Agosti 3 ni Simba Day ya 16 ambapo Uwanja wa Mkapa mashabiki wamejitokeza wengi na tiketi ilikuwa ni Sold Out mapema siku mbili kabla ya tukio.

Miongoni mwa waliopo Uwanja wa Mkapa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mo Dewji pia kulikuwa na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa ikiwa ni pamoja na King Kiba, Mwamba wa Kaskazini Joh Makini.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba amewashukuru mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye Simba Day na kutamblisha wacheza wa timu hiyo kuelekea msimu wa 2024/25 ambapo kutakuwa namchezo wa kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda.