GAMONDI: TUNAITANGAZA YANGA DUNIANI

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amebainisha kuwa uwepo wao Afrika Kusini una faida kubwa kutokana na kucheza mechi za ushindani ambazo ni muhimu kuelekea msimu mpya huku wakiitangaza timu hiyo duniani kote.

Gamondi aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuinoa Yanga yenye maskani yake Jangwani, Kariakoo inatarajiwa kurejea Bongo ikikamilisha mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs.

Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24 waligota nafasi ya kwanza na pointi 80 watapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Julai 28 watakuwa na kazi kwenye mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs.

Gamondi amesema: “Ujio wetu hapa Afrika Kusini umekuwa muhimu sana kwetu kwenye maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2024/25 na kucheza na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) ni sehemu ya kuendelea kuitangaza klabu yetu barani Afrika na Duniani kote.”

Ni Nasreddine Nabi yeye anainoa Kaizer Chiefs na aliwahi kuifundisha Yanga pia kabla ya kuondoka hapo kuwa sehemu nyingine kwa ajili ya kuendeleza kazi yake aipendayo.