DJUMA SHABAN AJIUNGA NA ‘WAUAJI WA KUSINI’ NAMUNGO KWA UHAMISHO HURU

BEKI wa zamani wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Djuma Shaban mwenye umri wa miaka 31 ametambulishwa kuwa mali ya Namungo.

Djuma ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amejiunga na ‘Wauaji wa Kusini’ Namungo FC akiwa ni mchezaji huru.

Nyota huyo mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia akiwa katika majukumu yake hivyo atakuwa kwenye changamoto mpya ndani ya Namungo FC.

Jezi ambayo amekabidhiwa kwa ajili ya kupambania majukumu yake mapya ni namba 21 atakayokuwa nayo kwa msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti 16 2024.