>

SEN KUJENGA UWANJA MWINGINE SIMBA

MPANGO mkubwa wa Simba kwa sasa ni kuendelea kuwa bora kwa kuboresha mazingira ya wachezaji ikiwa ni pamoja na sehemu ya kufanyia mazoezi.

Julai 14 2024 Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohammed Dewji alikutana na kufanya mazungumzo na Simba Executive Network (SEN).

SEN ni mtandao wa mashabiki wa Simba ambao huchangia ada ya 1,500,000 kwa mwaka kwa ajili ya miradi maalumu ya miundombinu ya klabu. Wanachama wa SEN hupata faida nyingi kama bima za maisha, tiketi za mechi na faida nyingine nyingi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa SEN akiwapo Mwenyekiti Abdulrazak Badru, Makamu wake Farouk Baghoza, Katibu Dkt. George Ruhago, Katibu Msaidizi Richard Mwalibwa na wanachama wa SEN. Menejimenti ya Simba iliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula.

Malengo ya Mwaka SEN inalenga kutengeneza uwanja wa mazoezi ili kuongeza idadi ya viwanja vya mazoezi Bunju.

Ikumbukwe kwamba kwa sasa Simba ipo kambini nchini Misri ambapo imeshakamilisha wiki moja ya maandalizi kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Agosti 3 2024 inatarajiwa kuwa siku maalumu ya utambulisho wa wachezaji wapya pamoja na wale waliokuwa kwenye kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24.