>

SIMBA WAPO KAMILI GADO KWA KAZI

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Simba wapo kamili gado kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza kati ya Agosti.

Ipo wazi kuwa msimu wa 2024/25 Simba iligotea nafasi ya tatu kwenye msimamo huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo.

Kwa sasa Simba ipo kambini nchini Misri chini ya Fadlu Davids ambaye ni kocha mkuu, kocha msaidizi, Darian Wilken, mchambuzi wa video, Mueez Kajee na kocha wa Viungo, Riedoh Berdien hawa tayari wapo Misri baada ya kuwasili kambini Julai 10.

Mwamba Selemani Matola ambaye ni kocha msaidizi aliwapokea wageni hao kwa ajili ya kuendelea na kazi ya kukisuka kikosi hicho kitakachopeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho katika anga la kimataifa hawataanzia hatua ya awali.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema: “Tupo tayari kwa ajili ya msimu mpya na benchi la ufundi linaendelea na kazi kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.’.