>

ONA PICHA ZA MAJEMBE MAPYA YA YANGA WAKIELEKEA MAZOEZINI

YANGA chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi tayari ipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti 2024.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa watetezi baada ya kufanikisha malengo hayo msimu wa 2023/24 walipomaliza wakiwa na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30.

Kwenye usajili wa dirisha kubwa imeongeza mastaa wapya ikiwa ni pamoja na Clatous Chama ambaye alikuwa ndani ya Simba msimu uliopita huku kiungo Aziz Ki naye akiongeza mkataba kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Gamodi amebainisha kuwa wanatambua wana kazi kubwa kwenye ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika maandalizi mazuri yanafanyika kuwa kwenye mwendo mzuri.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye ligi na Ligi ya Mabingwa kikubwa ni ushirikiano na tunaamini kwamba tutafanya vizuri.”

Julai 28, Yanga SC watakuwa nchini Afrika Kusini kushiriki Kombe la Toyota ambapo wacheza na Kaizer Chief iliyochini ya kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi.