>

MKUDE HATOKUWA SEHEMU YA KIKOSI CHA YANGA

KIUNGO wa kazi kwenye eneo la ukabaji ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi inatajwa kuwa hajaongeza bado mkataba.

Anaitwa Jonas Mkude ambaye kwenye maisha yake ya soka la ushindani amecheza timu kubwa mbili pekee mpaka sasa ya kwanza ilikuwa ni Simba kisha akaibuka ndani ya Yanga.

Ni msimu wa 2023/24 alikuwa ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kupewa Thank You na mabosi wa Simba kumpa ruhusa apate changamoto mpya.

Mkude anakumbukwa ndani ya Simba kwa mashuti yake magumu akiwa nje ya 18 na kutawala eneo la kiungo mkabaji aliwahi kuwa nahodha wa Simba kabla mikoba yake kupewa mwamba John Bocco.

Bocco naye hayupo kwa sasa ndani ya Simba msimu wa 2023/24 ulipogota mwisho hajaongezewa mkataba yupo ndani ya JKT Tanzania kwa ajili ya changamoto mpya.

Mazungumzo ya kuongeza mwaka Mwingine yalianza ila kocha Gamondi aliamua kusitisha na sasa rasmi wameachana nae.