>

GUEDE ASAINI SINGIDA BLACK STARS

MSHAMBULIAJI wa kimataifa Joseph Guede ametambulishwa na mabosi wa Singida Black Stars kwa ajili ya kupata changamoto mpya katika kikosi hicho.

Guede raia wa Ivory Coast alitambulishwa ndani ya Yanga kwenye dirisha dogo yeye ni raia wa Ivory Coast ambapo mpango mkubwa ilikuwa ni kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji.

Nyota mwingine ambaye alitambulishwa Yanga kwenye dirisha dogo ni Okra Magic ambaye huyu anaingia kwenye orodha ya nyota ambao watakutana na Thank You kutoka Yanga.

Guede amesaini mkataba wa kuitumikia Singida Black Stars wa mwaka mmoja akitokea ndani ya kikosi cha Yanga inayolewa na Kocha Mkuu Migue Gamondi.

Rekodi zinaonyesha kuwa akiwa ndani ya Yanga kwenye Ligi Kuu Bara nyota huyo alifunga mabao sita kati ya 71 yaliyofungwa na timu hiyo iliyomaliza msimu wa 2023/24 ikiwa namba moja na pointi 80.