>

MWAMBA JOHN BOCCO KUKIWASHA HUKU

MTAMBO wa mabao ndani ya uwanja John Bocco bado yupo sana uwanjani ambapo kwa msimu wa 2024/25 atakuwa ndani ya kikosi cha JKT Tanzania.

Ipo wazi kwamba Bocco ni mshambuliaji bora wa muda wote ndani ya Bongo akiwa amefunga zaidi ya mabao 100 kwenye ligi alianza kucheka na nyavu akiwa na Azam FC, Simba na sasa ni ndani ya JKT Tanzania.

Masau Bwire, Ofisa Habari wa JKT Tanzania amesema kuwa wanawachezaji wazuri ambao watakuwa na kazi kuwapa burudani mashabiki pamoja na kutafuta matokeo kwenye mechi za ushindani.

“Kwa sasa hakuna muda wa kupoteza tunaamini kwamba makipa watapata tabu ukizingatia tuna mshambuliaji wa mabao. Tupo tayari na tunafanya maboresho makubwa kwenye kikosi ukizingatia kwamba tuna wachezaji wazuri.

“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tupo tayari kwa ajili ya msimu mpya na imani yetu ni kwamba tutakuwa kwenye mwendo mzuri mwanzo wa ligi mpaka mwisho.”

Julai 10 2024 Bocco alitambulishwa kuwa ni mchezaji mpya ndani ya kikosi cha JKT Tanzania hivyo atakuwa hapo kwa msimu wa 2024/25.