>

MSTAAFU KIKWETE na MTOTO wa MANJI WAZUNGUMZA KWA UCHUNGU MAISHA ya MANJI HADI KUFARIKI…

Mtoto wa Marehemu Yusuf Manji, Mehbub amesema baba yake alikuwa akiipenda mno Klabu ya Yanga yenye makao makuu yake katika Mtaa wa Jangwani, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Amesema japokuwa ametangulia mbele za haki lakini bado moyo wake ameuacha Jangwani huku akieleza kuwa wakati mwingine walikuwa wakipata matokeo ya Yanga kwa kumtazama baba yao usoni, ikishinda alikuwa akifurahi sana lakini ikifungwa alikuwa akikasirika mno.