>

JEMBE AFICHUA ALIVYOMSHAURI MANJI AMSAJILI TAMBWE – VIDEO

MWANDISHI wa Habari na mchambuzi wa soka mahiri, Saleh Ally ‘Jembe’ amesema marehemu Yusuf Manji alikuwa rafiki yake wa karibu na kwamba ni yeye ndiye aliyemshauri amsajili mshambuliaji Amis Tambwe baada ya kuachwa na Simba.

Jembe ameyasema hayo Julai 7, 2024 kwenye dua maalum iliyoandaliwa na familia ya Marehemu Manji, iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.