MABINGWA wa Ligi Kuu England ni Manchester City baada ya kumaliza msimamo waliwa na pointi 91 tofauti ya pointi mbili na washika bunduki Arsenal.
Arsenal ilikuwa katika ubora wake ndani ya 2023/24 imegotea nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu England ambayo ushindani wake ni mwanzo mwisho.
Ipo wazi kuwa Mei 19 2024 ilikuwa ni mechi za mwisho za msimu na matokeo ya ushindi wa Manchester City 3-1 West Ham umewapa ubingwa kwa mara nyingine tena City.
Mabao ya City yalifungwa na Phil Foden dakika ya 2, 18 na Rodri dakika ya 59 bao la West Ham lilifungwa na Mohamed Kudus dakika ya 43.
Licha ya ushindi wa Arsenal 2-1 Everton bado ngoma ilikuwa nzito kwa washika bunduki hao na mabao yalifungwa na Takehiro Tomiyasu dakika ya 43 na Kai Havertz dakika ya 89 na bao la Everton lilifungwa na Idrissa Gueye dakika ya 40.
Liverpool ni namba tatu ikiwa na pointi 82 zote zimecheza mechi 38 msimu wa 2023/24 kazi mpya inatarajiwa kuanza kwa msimu wa 2024/25 kujua nani atakuwa nani.