Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika imemalizika kwa sare tasa katika dimba la Olympique Hammadi Agrebi (Radès) kati ya Mabingwa mara nne Esperance Tunis dhidi ya Mabingwa mara 11 Al Ahly ya Misri.
FT: Esperance ?? 0-0 ?? Al Ahly
Mchezo wa fainali ya pili utakaopigwa Mei 25, 2024 katika dimba la Al Salam, Cairo utaamua timu itakayotwaa ubingwa huo.