>

SHIRIKISHO LA SOKA LA ALGERIA LINAPANGA KUJIONDOA CAF

Shirikisho la soka la Algeria sasa linapanga kujiondoa ndani ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) na kujiunga na Shirikisho la soka la Asia (AFC) kwa kuwa wanaamini CAF haijawahi kuwatendea haki katika maamuzi muhimu katika soka la Afrika.

Pia walitaja kilichotokea hivi juzi kati ya RS Berkane na USM Alger kama moja ya sababu zinatakazosababisha wao kujiondoa.

AFC ilianzishwa mwaka wa 1954 na ina wanachama 47 na ikiwa Algeria itakubaliwa, itakuwa wanachama 48.