YANGA BINGWA MARA 30 LIGI KUU BARA

YANGA chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2023/24 baada ta kufikisha pointi 71 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote Bongo.

Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibw Sugar umewapa taji hilo la 30 wakitwaa mara tatu mfululizo wakiwa ni watawala katika zama za sasa.

Licha ya Mtibwa Sugar kuanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Ilanfya dakika ya 32, kipindi cha pili mzani ulikwekwa sawa kupitia kwa Kennedy Musonda dakika ya 66 na kamba ya tatu ikafungwa na Clement Mzize dakika ya 81.

Mtibwa Sugar wanabakiwa na pointi 20 wakipambana kupata matokeo katika mechi zinazofuata ili wasishuke daraja.

Mechi tatu Yanga ipo nazo mkononi kukamilisha msimu wa 2023/24.

Ikumbukwe kwamba vita ya ubingwa imegota mwisho kuna ile ya kiatu cha ufungaji bora Aziz KI wa Yanga na Feisal Salum wa Azam FC hawa wametupia mabao 15.