ULINZI UNYAMANI NI PASUA KICHWA

NDANI ya tatu bora msimu wa 2023/24 kikosi cha Simba kwenye ulinzi ni pasua kichwa baada ya kucheza mechi 25 kwenye mechi za ushindani.

Ni Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza unaingia kwenye orodha ya mchezo ulikusanya mabao mengi kwa Simba mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo huo ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga na pointi tatu zikaenda ugenini kwa kuwa Simba ilikuwa nyumbani. Ukuta wa Simba umeruhusu jumla ya mabao 23 wakikusanya pointi 56 kibindoni ndani ya ligi.

Namba moja kwa kuruhusu mabao machache ni Yanga iliyokusanya jumla ya mabao 12 inafuatiwa na Azam FC iliyoruhusu mabao 19.

Mchezo unaofuata kwa Simba itakuwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba kusak pointi tatu ugenini Mei 12.