KYLIAN MBAPPÉ ATHIBITISHA KUWA ATAONDOKA PSG

Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappé amethibitisha kuwa ataondoka klabuni hapo mwisho wa msimu huu. Mbappé amesema hayo kupitia picha jongeo kwenye mitandao ya kijamii ingawa hajabainisha ni wapi ataelekea.

Paris Saint-Germain hawajamjumuisha Kylian Mbappe kwenye chapisho la mtandao wa kijamii wakitangaza jezi zao mpya hali inayoashiria kuwa nyota huyo raia wa Ufaransa hayupo kwenye mipango yao ya msimu ujao.

Inaaminika kuwa mfungaji huyo wa muda wote wa PSG tayari amefikia makubaliano ya kujiunga na vigogo wa Uhispania, Real Madrid ingawa hakuna klabu iliyoweka bayana ukweli huo.

Baadhi ya wachezaji wa PSG wameonekana kwenye chapisho la la klabu hiyo kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na jezi hizo mpya, wakiwemo Marquinhos, Nuno Mendes na Lucas Hernandez lakini Mbappe hakuonekana.