MASTA GAMONDI AJA NA HILI BAADA YA KUTOSHANA NGUVU NA MAMELODI

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa amefurahishwa na utendaji wa kazi wa wachezaji wake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Kitendo hicho ni sawa na kuwapa tano wachezaji wake huku wakipiga hesabu za kupata ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa pili ugenini utakaoamua nani ni nani atakeyetinga hatua ya nusu fainali.

Machi 30 ubao wa Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali baada ya dakika 90 ulisoma Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilianza mchezo huo ikiwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha kwanza wakikosa huduma ya profesa Pacome, Yao Yao ambao hawa hawakuwa fiti.

Gamondi amesema: “Nimefurahishwa na uwezo wa wachezaji wa timu yangu kwa kuwa kila mmoja alijitoa kwenye kutimiza majukumu yake licha ya kwamba kuna nafasi ambazo tulishindwa kuzitumia.

“Bado kuna nafasi ya kufanyia kazi makosa kwa kuwa kuna mchezo mwingine ambao tutacheza dhidi yao, tuna matumaini yakufanya vizuri mchezo ujao.

“Kila mmoja ameona namna ambavyo wachezaji wamejituma na hilo ni jambo kubwa wanastahili pongezi na kufanya kazi kubwa zaidi kwa mechi zinazofuata,”.